Friday, April 19, 2013

BMU NI WASIMAMIAJI WA RASILMALI ZA ZIWA AU WATAWALA ?


            

Vikundi vya kusimamia rasilmali za ziwani maarufu kama BMU ni vikundi vya wadau vilivyoundwa kisheria kwa dhumuni la kusaidiana na Serikali katika zoezi zima la kuhifadhi mazingira ya mialo,kushirikisha wavuvi katika kuhakikisha kuwa rasilmali zote za  samaki zinahifadhiwa kwa manufaa ya taifa.

Vikundi hivi kulingana na malengo ya kuanzishwa kwao yalijikita katika kuhakikisha ufuatiliaji endelevu wa kudhibiti uvuvi haramu unakuwepo na hivyo endapo zoezi hilo lingefanikiwa uchumu wa taifa ungeliimarika hususan bidhaa yote itokanayo na samaki iwapo  ingelipitia katika utaratibu mzima wa kiserikali.

Aidha huenda pengine nao wahusika katika kuhakikisha kuwa shughuli za vikundi hivyo hawana mwanga wa kutosha ya kwamba wao inawabidi wafanye nini ndio maana kazi zao zinaonekana hafifu kiasi kuwa uvuvi huo haramu unaonekana kushamiri katika baadhi ya mialo ya kanda ziwa.Uendelevu wa kuwepo kwa zana haramu za uvuvi katika vijiji vya wavuvi ni jambo linaloonyesha ulegevu wa wazi wa vikundi vya BMU.

Huenda pengine serikali haijui kwa undani ni kwa vipi vikundi hivi licha ya kuwezeshwa kikazi na kimaadili lakini bado wanakwepa wajibu na kuviacha viwanda vya samaki vikanyang’anywa mali ghafi hadharani  na huku zikielekea wakati mwingine katika nchi jirani.Nchi hii ni yetu ni wajibu serikali yetu ikashauriwa na kutahadharihwa kwa hili.

Vikundi vya BMU inabidi viendeshwe kwa kuzingatia kanuni zake na viongozi wake kuzigatia mapashwa yao ambayo ni kuwa kama mawakala wa serikali atika upande huo wa uimaishaji wa uchumi wan hi yetu.

Kinyume na hayo viongozi wengi katika mialo mbalimbali wameachana na makusudio ya wajibu wan a kujiingiza katika mambo kiutawala,kuamua mashauri ya wakazi wa maeneo yao hata kama mashauri hayo  hayahusiani kamwe na masuala ya ziwani kama vile magomvi ya kifamilia,kutoza tozo za mashauri hayo,kunyan’anya ardhi,kuwanyanyasa wananchi au wavuvi kwa kuwafukuza katika makazi yao,kuharibu mazao yao hasa iwapo mhusika ameonyesha kutokukubaliana na utaratibu wa viongozi hao. Hivyo muda mwingi unaishia katika mambo ya kiutawala.

Kanini za BMU zinaeleza wazi kuwa vikundi hivyo vitafanya kazi chini ya uongozi wa Serikali za vijiji au mitaa ziliko.Kwa hali halisi ilivyo kanuni hizo ni ndoto kwani viongozi wa vikundi hivyo wamekuwa wakijiingiza katika kuwadharau viongozi wa vijiji na kujifanya wao kuwa watawala.Vurugu nyingi zimekuwa zikibainishwa katika kambi za wavuvi viongozi wa vikundi hivyo wakijifanya miungu.

Taratibu za aina hiyo ndicho chanzo cha ukwamishaji wa shughuli za usimamizi na ufuatiliaji wa wavuvi haramu na wao kushindwa kuripoti vitendo hivyo serikalini na kwa wakati na hivyo kuwepo kwa takwimu za ubabaishaji za doria zilizoendeshwa.K
a.
.Kusimamia miradi midogo midogo ya kiuchumi kwa manufaa ya jamii ya wavuvi.
.Kuendesha doria za mara kwa mara dhidi ya uvuvi harramu.
Kwa upande mwingine kanuni hizo zinataja dhahiri kuwa chini ya Sheria za Serikali za mitaa Na.7 na 8 za mwaka 1982,vikundi hivyo vitaundwa kama vikundi vingine katika kijiji au Mtaa na vitaendesha shughuli zake chini ya serikali hizo za vijiji au mitaa.
Tofauti na muongozo huo wa vikundi vya BMU baadhi ya viongozi wa vikundi hivyo wanaacha kuendana na wajibu wao badala yake wanabaki kusigana na Halmashauri za vijiji juu ya mambo ya kiutawala.