Vikundi vya kusimamia rasilmali za ziwani maarufu kama BMU
ni vikundi vya wadau vilivyoundwa kisheria kwa dhumuni la kusaidiana na
Serikali katika zoezi zima la kuhifadhi mazingira ya mialo,kushirikisha wavuvi
katika kuhakikisha kuwa rasilmali zote za
samaki zinahifadhiwa kwa manufaa ya taifa.
Vikundi hivi kulingana na malengo ya kuanzishwa kwao
yalijikita katika kuhakikisha ufuatiliaji endelevu wa kudhibiti uvuvi haramu
unakuwepo na hivyo endapo zoezi hilo lingefanikiwa uchumu wa taifa
ungeliimarika hususan bidhaa yote itokanayo na samaki iwapo ingelipitia katika utaratibu mzima wa
kiserikali.
Aidha huenda pengine nao wahusika katika kuhakikisha kuwa
shughuli za vikundi hivyo hawana mwanga wa kutosha ya kwamba wao inawabidi
wafanye nini ndio maana kazi zao zinaonekana hafifu kiasi kuwa uvuvi huo haramu
unaonekana kushamiri katika baadhi ya mialo ya kanda ziwa.Uendelevu wa kuwepo
kwa zana haramu za uvuvi katika vijiji vya wavuvi ni jambo linaloonyesha
ulegevu wa wazi wa vikundi vya BMU.
Huenda pengine serikali haijui kwa undani ni kwa vipi
vikundi hivi licha ya kuwezeshwa kikazi na kimaadili lakini bado wanakwepa
wajibu na kuviacha viwanda vya samaki vikanyang’anywa mali ghafi hadharani na huku zikielekea wakati mwingine katika
nchi jirani.Nchi hii ni yetu ni wajibu serikali yetu ikashauriwa na
kutahadharihwa kwa hili.
Vikundi vya BMU inabidi viendeshwe kwa kuzingatia kanuni
zake na viongozi wake kuzigatia mapashwa yao ambayo ni kuwa kama mawakala wa
serikali atika upande huo wa uimaishaji wa uchumi wan hi yetu.
Kinyume na hayo viongozi wengi katika mialo mbalimbali
wameachana na makusudio ya wajibu wan a kujiingiza katika mambo
kiutawala,kuamua mashauri ya wakazi wa maeneo yao hata kama mashauri hayo hayahusiani kamwe na masuala ya ziwani kama
vile magomvi ya kifamilia,kutoza tozo za mashauri hayo,kunyan’anya
ardhi,kuwanyanyasa wananchi au wavuvi kwa kuwafukuza katika makazi yao,kuharibu
mazao yao hasa iwapo mhusika ameonyesha kutokukubaliana na utaratibu wa
viongozi hao. Hivyo muda mwingi unaishia katika mambo ya kiutawala.
Kanini za BMU zinaeleza wazi kuwa vikundi hivyo vitafanya
kazi chini ya uongozi wa Serikali za vijiji au mitaa ziliko.Kwa hali halisi
ilivyo kanuni hizo ni ndoto kwani viongozi wa vikundi hivyo wamekuwa
wakijiingiza katika kuwadharau viongozi wa vijiji na kujifanya wao kuwa
watawala.Vurugu nyingi zimekuwa zikibainishwa katika kambi za wavuvi viongozi
wa vikundi hivyo wakijifanya miungu.
Taratibu za aina hiyo ndicho chanzo cha ukwamishaji wa
shughuli za usimamizi na ufuatiliaji wa wavuvi haramu na wao kushindwa kuripoti
vitendo hivyo serikalini na kwa wakati na hivyo kuwepo kwa takwimu za
ubabaishaji za doria zilizoendeshwa.K
a.
.Kusimamia miradi midogo midogo ya kiuchumi kwa manufaa ya
jamii ya wavuvi.
.Kuendesha doria za mara kwa mara dhidi ya uvuvi harramu.
Kwa upande mwingine kanuni hizo zinataja dhahiri kuwa chini
ya Sheria za Serikali za mitaa Na.7 na 8 za mwaka 1982,vikundi hivyo vitaundwa
kama vikundi vingine katika kijiji au Mtaa na vitaendesha shughuli zake chini
ya serikali hizo za vijiji au mitaa.
Tofauti na muongozo huo wa vikundi vya BMU baadhi ya
viongozi wa vikundi hivyo wanaacha kuendana na wajibu wao badala yake wanabaki
kusigana na Halmashauri za vijiji juu ya mambo ya kiutawala.
No comments:
Post a Comment