NYUMBA TANO ZACHOMWA MOTO
(na Gilbert
J Makwabe)
Jeshi la polisi mkoani Kagera linachunguza tukio la uchomaji
moto nyumba zipatazo nne na jiko moja tukio lililotokea hivi karibuni katika
vitongoji vya Bushaigi na Ruhanga,kijiji ch a Bumai,Kata Kishanji wilayani
Bukoba kwa tuhuma za uchawi.
Kwa mujibu
wa kamanda wa polisi mkoani Kagera Henry Salewi nyumba zilizochomwa moto na
wananchi waliojiita wenye hasira kali ni mali yam zee Cleophace
Tiruirukwa(miaka 67) ambamo waliishi jumla ya watu 8,nyumba ya
bintiyeErnestinaCleophaceambamo waliishi watu 5,nyumba ya mwanae wakiume Dennis
Cleophace ambamo waliishi watu4. Nyumba nyigine ni ya mweyekiti wa kitongoji
Costantine Cosmas pamoja na jiko moja.
Kamanda Salewi
aliwaambi waandishi wa habari kuwa hadi wakati huo watu wawili walikuwa
wanashikiliwa na polisi kutokana na
tukio hilo nao ni Christopher Nshoga(miaka 47) naLeopold
Kabigumila(miaka76).Mkuu huyo wa polisi alitoa wito kwa raia kuacha kujichukulia
sheria mikononi.
Habari zaidi
kutoka kijijini humo ni kuwa mzee Cleophace alituhumiwa na wanakijiji wenzake
kuwa aliwaloga watoto wa jirani yake na kuwa kwa sasa watoto hao wanaishi na
bibi yao kwani wazazi wao(baba na mama)walifariki siku nyingi baada ya kuugua
muda mrefu. Inasemekana pia kuwa watoto hao(ajina yamehifadhiwa) wamekuwa
wakiugua ugua kia wakati ila hwakuwa wamepelekwa hospitalini siku nyingi ila tu
kwa waganga wa kienyej.
Matukio hayo ya
wananchi kuwadhuru wenzao kwa imani za kishirikina yamezidi kushamiri mkoani
Kagera.Siku chache zilizopita yameshuhudiwa pia matukio kadhaa katika maeneo
tofauti.Tukio moja limejitokeza katika kijiji cha Kabajuga,kitongoji
Nyakabumba\Nyakiziba,kata ya Kasharu
wilaya ya Bukoba ambapo ilisemekana kuwa watuu wasiojulikana walivamia
kaya ya mwanakijijiTwaha Ramdhani(miaka51),wakifyeka mashamba yake na kuchoma
moto nyumba ambapo mali na mifugo viliteketea.
Tukio jingine
nmi lile lililotokea katika kijiji cha Kantare,kata Bwanjai wilayani Missenyi
ambapo nyumba ya Bw.Petro Kakwama(miaka70) ilitiwa moto na watu wasiojulikana
na huku wajukuu zake6 alioishi nao nyumbani humo waliungua vibaya. Watoto hao
ni Frank Leonard(3),Livinus Donati(2),Leonard Antidius(7),Anitha
Dominic(17),Alli Mussa(6) na Dennis Dominic(14). Uchomaji wa nyumba hiyo pia
inasemekana kuhusishwa na imani za kishirikina.
_mwisho_