Saturday, March 3, 2012

KAHWA YANYAUKA UCHUMI WA WAKULIMA HATARINI


(Na Gilbert J. Makwabe)

TAASISI ya utafiti wa zao la Kahawa(TaCRI)kanda ya Maruku mkoani Kagera,imelenga kuzalisha jumla ya miche ya kahawa zidi ya 3.5 milioni,ambayo itasambazwa kwa wakulima wa zao hilo ndani ya kanda ya ziwa Viktoria.

Akiongelea juu ya uzalishaji huo,hivi karibuni meneja wa TaCRI kanda ya ziwa bw.Nyabis Ng'homa,uzalishaji huo ni sehemu ya malengo ya taasisi hiyo kwa mwaka huu.


Bw.Ng'homa alifafanua kuwa miche hiyo imelengwa kuzalishwa katika vitalu vilivyoko katika wilaya za Bukoba vijijini,Missenyi,Muleba,Karagwe,Biharamulo na Ngara.


Vitalu vingine vitakavyosalisha miche hiyo ni katika wilaya za Ukerewe,Sengerema na Geita.Ambavyo idadi ya miche itakayokuwa imezalishwa katika vitalu hivyo
  inakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 3.5 ambayo itasambazwa  kwa wakulima.

Wakati huo huo,wakulima mkoani hapa,wameshauriwa kujenga utamaduni wa kutembelea kituo cha utafiti wa kilimo Maruku ili kupata ushauri wa kilimo bora pamoja na mbegu bora.


Kahawa limeendelea kuwa ni zao kuu la biashara mkoani Kagera lakini hivi sasalinazidi kudorora kutokana na kupungua kwa mashina ya mibuni mashambani kutokana na mamlaka husika hususan chama cha ushirika cha KCU(1990)Ltd kutokuwa na mikakati madhubuti ya
  kumkaribia  mkulima katika kazi yake ya kilimo cha kahawa shambani,aidha kwa mikopo nafuu na isiyo na ugumu wa kuipata. Kwa hali hiyo wkulima washindwa kupata pembejeo kama vile samadi na nyingine mintarafu zao hilo.Kutokana  na uchumi mdogo wa wakulima hao uchunguzi umeonyesha kuwa baadhi ya mashamba ya kahawa mkoani humo yameonekana kukanda na kuonyesha kushambuliwa na wadudu kama vile sisimizi nawengine.

Tatizo kubwa ambalo linaonekana kuyakabili mashamba ya wakulima kwa sasa ni ugonjwa wa MNYAUKO wa mibuni ambapo mibuni inazidi kunyauka mashambani kila kukicha.Pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na wataalam wa kilimo katika mkoa kwa kushirikiana na kituo cha utafiti Maruku ili kutatua tatizo hilo,kwa nafsi ya mkulima uchumi wake unahofiwa kuwa hatarini.

MWISHO

No comments:

Post a Comment