Na Gilbert J.Makwabe
Wakati tume ya taifa ya kutafuta maoni ya wananchi juu ya upatikanaji wa katiba mpya nchini chini ya uongozi wa jaji Joseph Warioba ilipouzuru mkoa wa Kagera hivi karibuni kutafuta maoni hayo wanahabari mkoani humo waliyanukuu baadhi ya maoni ya wananchi ambayo yalielekea kupata msisitizo katika mikutano mbalimbali.Maoni hayo ni kama vile:
.Suala la uwepo wa mgombea binafsi wakati wa uchaguzi.
.Matokeo ya uchaguzi wa Rais kuweza kuhojiwa mahakamani inapobidi kufanya hivyo.
.Uwepowatume huru ya uchaguzi
.Kupunguza madaraka ya Rais
.Katiba iweze kuonyesha nchi inafuata siasa gani kama sio ya ujamaa na kujitegemea.
Kufutwa kwa nafasi za makamu wa rais,wakuu wa wilaya namikoa.
.Jaji Mkuu aweze kuteuliwa na jopo la majaji.
.Wenyeviti wa vijijina mitaa walipwe mishahara.
.Serikali ya Tanzania iwe ni moja,rais mmoja na bunge moja.
.Mawaziri wasitokane na wabunge ila watu waiombe kama kazi na pia kila waziri awe na taaluma na nafasi atakayooba.
.Kifungu cha 19 cha katiba ya sasa kuhusu uhuru wa kuabudu kibaki kilivyo na kuwa serikali isijiingize katika shughuli zozote za kidini wala kukifadhili kikundi chochote cha aina hiyona kuwaiwaache wananchi wafuate itikadi za kidini wazitakazo na kuwa kiwepo kifungu kinachozuia dhehebu moja kulikashifu dhehebu jingine.Pia kuwepo na kifungu kinacholibana dhehebu litakalotoa mahubiri yatakayochochea chuki,vurugu na kuvunja amani ya wananchi.
.Kupinga ndoa za jinsia moja
.Ardhi kubaki mikononi mwa wananchi.
.Kudhibitiwa kwa ada za shule binafsi na kufutwa kwa ada za vyuo vya elimu ya juu.
.Kuruhusiwa kwa mahakama ya kadhi na kuwa serikali igharimie shughuli za mahakama hiyo na kwamba taifa liruhusiwe na katiba kujiunga na shirika la kimataifa la kiislamu-OIC.
.Kuwepo kwa utetezi kuanzia mahakama za mwanzo na kuwa iwepo kada ya mawakili wa kuwatetea wananchi kwa ngazi hiyo.
,Suala la ufisadi na ubaadhirifu wa rasilmali za taifa udhibitiwe na katiba mpya.
.Adhabu ya kifo ibaki pale pale kwa watu wanaua wenzao maksudi na kutiwa hatiani.
.liundwe baraza la seneti ambalo litawajumuisha waasisi wa taifa kamailivyo kwa uigereza na marekani jukumu lake kubwa nikuishauri serikali kuhusu maamuzi magumu ya kitaifa.
No comments:
Post a Comment