Friday, August 10, 2012

Mgawanyo wa majukumu kijinsia unabadilisha mwelekeo wa utamaduni?

Na Gilbert J.Makwabe

Mbali ya tofauti mbali mbali zilizokuwepo kati ya jamii moja na nyingine hapa nchini na Africa kwa ujumla wake lakinijamii iliyokubwa huelekeana katika mila na desturi zao.

Mathalani nafasi ya mwanamke na mtotoau mume na familia yake siku hizi inaelekea kubadilika kwa kiwango kikubwa,pengine hiyo ikiwa ni hatua muhimu sana kwa dunia kutaka kuubadilisha mfumo dume kuelekea usawa wa kijinsia.

Lakini siamini kuwa desturi zote za kale zilikuwa mbovu kwa sababu kila mmoja alikuwa na jukumu lake la kutimiza na kuwa kila upande kuwa na haki zake,kwa mfano motto alikuwa na haki ya kunyonyeshwa na mama yake hadi hapo ambapo alikuwa amefikisha umri wa kuachishwa ziwa.

Lilikuwa nijukumu la mwanamume kujenga nyumba kwaajili ya familia,kuoa,kuitunza na kuilinda familia yake.

Hapo kale  mama alikuwa na jukumu la kuilisha familia baada ya kusaidiana na baba na watoto katika uzalishaji wa chakula hicho wakitofautiana katika masaa ya kufanya kazi mashambani.

Pengine mfumo huo uliendana na taratibu za kiutawala uliokuwepo wakati ule kitu ambacho tunaweza tukakiita kuwa ni mfumo gandamizi.

Watoto walikuwa ni fahari ya familia huku wakiwa ni sehemu muhimu sana katika ukamilishaji majukumu kati ya baba namama huku wakiendeleza kizazi cha kiukoo,kuwa msaada mkubwa kwa wazazi hasa walipokuwa wamezeeka.

Ndoa ziliratibiwa na wazazi huku kila upande ukitaka kujua undani wa habari zihusuzo tabia na taratibu za kuishi baina ya familia za pande zote yaani upande wa msichana na ule wa mvulana.

Utamaduni huo ulikuwa na faida ya kuwahakikishia wanandoa usalama na amani kimaisha,ambapo utamaduni wa kutozwa kwa mahari kwa upande wa mume ni jambo lililompatia heshima binti asionekane ni binadamu wa wakuozwa kama mtumwa.

Desturi ya umiliki wa watoto kwa upande wa mume au mke kulingana na taratibu za makabila ya kiafrika  iliasisiwa na mababu zetu ili kila mmoja aujue ubini wake,ukoo na eneo atokako.

Jambo hili lililandana na hali ya malezi kwa watoto,watoto watambue taratibu adili za kufuata kama vile kuwaheshimu wakubwa na kuwasikiliza pale walipotoa nasaha zao na hilo halikuwa na ubaya wowote tofauti na hali ya siku hizi.

Zamani za mabibi zetu hata kama shule zilikuwa tayari zimeanzishwa lakini sio wasichana wengi walikuwa wameandikishwa shuleni hata hivyo hali  hiyo ilikuwa haimwondolei mtu hali ya kutambua mema na mabaya ya maisha,ingawa kwa sasa hatupaswi kuendelea na hali ya kutojua kusoma na kuandika.

Dunia ya sasa inahitaji kisomo na hata mtoto afike chuo kikuu wote  wa kike au wa kiume wafanye kazi sawa kama ilivyo sasa,lakini methali hutuambia hivi  mkataa mila ni mtumwa. 

Maana ni budi tuziishi zile taratibu nzuri na za utu tulizoelekezwa zamani na wazazi wetu,mfano kunawa mikono kabla na baada ya kula,kuwaamkia watu,kuonyesha heshima kwa kila mtu,kuonyesha hali ya utii kwa wakubwa,kujibu kila swali tuulizwapo na kwa unyenyekevu na mengine kama hayo,kwani hata kama utakuwa umeajiriwa kazi uadilifu wako kutokana na malezi uliyopewa na wazazi kila mara humvutia muajiri.

Taratibu za ubebaji mimba utunzaji wa mimba hizo miongoni mwa akina mama zinautofauti mkubwa kati ya zamani na siku hizi kwani zamani mama hakupewa uangalizi mkubwa kama ilivyo leo hii hasa kwa upande wa lishe na kiafya kwani hata pale mimba ilivyoendelea kukua ndivyo kazi zilivyendeleana vifo vya mapema kwa wtoto wachanga.

Changamoto nyingine ilikuwa ni kwa watu kuona fahari ya kuzaa watoto wengi tofauti na hali ya sasa kuwa wazazi wapange idadi ya watoto wa kuzaa! 

Siku hizi ni lazima wazazi wajadili fursa kati ya mimba na mimba ili mama aweze kupumzika kabla ya kubeba mimba nyingine.

Zamani njia nzuri iliyotumika kifamilia ni kwa mume na mke kuachana kwa muda ambapo kutokanana adha za mama baada ya kuzaa kama vile kutokwa na damu nyingi na kupungukiwa na nguvu mwilini ziweze kupungua.

Desturi nyingine za zamani na hata siku hizi zinatia shaka na kusababisha maswali yasiyokuwa na majibu miongoni mwa jamii hapa Afrika Mashariki,mathalani mbali ya kabila la Wahaya hakuna kabila jingine lolote ambalo wanaume wake wanakubali jukumu la kuchanja kuni kwaajili ya kupikia.

 Makabila yaliyo mengi ya kiafrika yaliamini kuwa jukumu la kuchanja kuni lilikuwa ni la wanawake kwa sababu wanawake ndio waliokuwa na jukumu la kupika chakula cha familia hivyo kuni ni kitendea kazi chao.
Na hata tukiyafuatilia baadhi ya makabila mengine kandokando ya ziwa Viktoria utakuta kuwa hata jukumu la kutafuta kitoweo mfano samaki kwaajili ya mboga ambapo ilibidi mama apeleke mazao ya chakula kwa wavuvi apate kubadilishana na samaki ndipo aweze kukamilisha mlo wa familia.

Hata hivyo mambo mengine yatahitaji makubaliano kati ya jinsiazote mbili kwani kwa upande wa kabila la Wahaya na jukumu la kuchanja kuni sababu zinazotolewa na wazee ni kuwa jambo hilo lilisababishwa na wanaume kuwaonea huruma wake zao wasiende porini kutafuta kuni kwani zamani ilikuwepo misitu minene yyenye wanyama wakali kama vile chui,chatu,samba na wengine ambao wangeliwadhuru na huku pengine wanawake hao wakiwa wamewabeba watoto migongoni,na kuwa hata hivyo wanaume walionekana ni jasiri na wakakamavu zaidi ukiwalinganisha na wanawake. 

Wakati Fulani mwandishi wa makala haya akihudhuria mafunzo huko Kampala,Uganda mafunzo yaliyowajumuisha washiriki kutoka maeneo tofauti ya Afrika Mashariki  suala la mwanamume kubeba jukumu la kuchanja kuni lilipelekea kuwashangaza wote!

Wananchi wa Kagera walitoa maoni gani kuhusu katiba mpya?

Na Gilbert J.Makwabe

Wakati tume ya taifa ya kutafuta maoni ya wananchi juu ya upatikanaji wa katiba mpya nchini chini ya uongozi wa jaji Joseph Warioba ilipouzuru mkoa wa Kagera hivi karibuni kutafuta maoni hayo wanahabari mkoani humo waliyanukuu baadhi ya maoni ya wananchi ambayo yalielekea kupata msisitizo katika mikutano mbalimbali.Maoni hayo ni kama vile:

.Suala la uwepo wa mgombea binafsi wakati wa uchaguzi.

.Matokeo ya uchaguzi wa Rais kuweza kuhojiwa mahakamani inapobidi kufanya hivyo.

.Uwepowatume huru ya uchaguzi

.Kupunguza madaraka ya Rais

.Katiba iweze kuonyesha nchi inafuata siasa gani kama sio ya ujamaa na kujitegemea.

Kufutwa kwa nafasi za makamu wa rais,wakuu wa wilaya namikoa.

.Jaji Mkuu aweze kuteuliwa  na jopo la majaji.

.Wenyeviti wa vijijina mitaa walipwe mishahara.

.Serikali ya Tanzania iwe ni moja,rais mmoja na bunge moja.

.Mawaziri wasitokane na wabunge ila watu waiombe kama kazi na pia kila waziri awe na taaluma na nafasi atakayooba.

.Kifungu cha 19 cha katiba ya sasa kuhusu uhuru wa kuabudu kibaki kilivyo na kuwa serikali isijiingize katika shughuli zozote za kidini wala kukifadhili kikundi chochote cha aina hiyona kuwaiwaache wananchi wafuate itikadi za kidini wazitakazo na kuwa kiwepo kifungu kinachozuia dhehebu moja kulikashifu dhehebu jingine.Pia kuwepo na kifungu kinacholibana dhehebu litakalotoa mahubiri yatakayochochea chuki,vurugu na kuvunja amani ya wananchi.

.Kupinga ndoa za jinsia moja  

.Ardhi kubaki mikononi mwa wananchi.

.Kudhibitiwa kwa ada za shule binafsi na kufutwa kwa ada za vyuo vya elimu ya juu.

.Kuruhusiwa kwa mahakama ya kadhi na kuwa serikali igharimie shughuli za mahakama hiyo na kwamba taifa liruhusiwe  na katiba kujiunga na shirika la kimataifa la kiislamu-OIC.

.Kuwepo kwa utetezi kuanzia mahakama za mwanzo na kuwa iwepo  kada ya mawakili wa kuwatetea wananchi kwa ngazi hiyo.

,Suala la ufisadi na ubaadhirifu wa rasilmali za taifa udhibitiwe na katiba mpya.

.Adhabu ya kifo ibaki pale pale kwa watu wanaua wenzao maksudi na kutiwa hatiani.

.liundwe baraza la seneti ambalo litawajumuisha waasisi wa taifa kamailivyo kwa uigereza na marekani jukumu lake kubwa nikuishauri serikali kuhusu maamuzi magumu ya kitaifa.

.Kuhusu uraia wa wageni ni kuwa raia wa kuandikishwa wasiruhusiwe kugombea uongozi katika nchi

Wednesday, March 28, 2012

NYUMBA TANO ZACHOMWA MOTO
           (na Gilbert J Makwabe)
Jeshi la polisi mkoani Kagera linachunguza tukio la uchomaji moto nyumba zipatazo nne na jiko moja tukio lililotokea hivi karibuni katika vitongoji vya Bushaigi na Ruhanga,kijiji ch a Bumai,Kata Kishanji wilayani Bukoba kwa tuhuma za uchawi.
            Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Kagera Henry Salewi nyumba zilizochomwa moto na wananchi waliojiita wenye hasira kali ni mali yam zee Cleophace Tiruirukwa(miaka 67) ambamo waliishi jumla ya watu 8,nyumba ya bintiyeErnestinaCleophaceambamo waliishi watu 5,nyumba ya mwanae wakiume Dennis Cleophace ambamo waliishi watu4. Nyumba nyigine ni ya mweyekiti wa kitongoji Costantine Cosmas pamoja na jiko moja.
        Kamanda Salewi aliwaambi waandishi wa habari kuwa hadi wakati huo watu wawili walikuwa wanashikiliwa  na polisi kutokana na tukio hilo nao ni Christopher Nshoga(miaka 47) naLeopold Kabigumila(miaka76).Mkuu huyo wa polisi alitoa wito kwa raia kuacha kujichukulia sheria mikononi.
      Habari zaidi kutoka kijijini humo ni kuwa mzee Cleophace alituhumiwa na wanakijiji wenzake kuwa aliwaloga watoto wa jirani yake na kuwa kwa sasa watoto hao wanaishi na bibi yao kwani wazazi wao(baba na mama)walifariki siku nyingi baada ya kuugua muda mrefu. Inasemekana pia kuwa watoto hao(ajina yamehifadhiwa) wamekuwa wakiugua ugua kia wakati ila hwakuwa wamepelekwa hospitalini siku nyingi ila tu kwa waganga wa kienyej.
      Matukio hayo ya wananchi kuwadhuru wenzao kwa imani za kishirikina yamezidi kushamiri mkoani Kagera.Siku chache zilizopita yameshuhudiwa pia matukio kadhaa katika maeneo tofauti.Tukio moja limejitokeza katika kijiji cha Kabajuga,kitongoji Nyakabumba\Nyakiziba,kata ya Kasharu  wilaya ya Bukoba ambapo ilisemekana kuwa watuu wasiojulikana walivamia kaya ya mwanakijijiTwaha Ramdhani(miaka51),wakifyeka mashamba yake na kuchoma moto nyumba ambapo mali na mifugo viliteketea.
       Tukio jingine nmi lile lililotokea katika kijiji cha Kantare,kata Bwanjai wilayani Missenyi ambapo nyumba ya Bw.Petro Kakwama(miaka70) ilitiwa moto na watu wasiojulikana na huku wajukuu zake6 alioishi nao nyumbani humo waliungua vibaya. Watoto hao ni Frank Leonard(3),Livinus Donati(2),Leonard Antidius(7),Anitha Dominic(17),Alli Mussa(6) na Dennis Dominic(14). Uchomaji wa nyumba hiyo pia inasemekana kuhusishwa na imani za kishirikina.
_mwisho_

Saturday, March 3, 2012

UCHUMI WA WAKULIMA KAGERA HATARINI

Kitalu cha miche bora ya kahawa (kutoka katika mtandao)

(Na Gilbert J. Makwabe)

 TAASISI ya utafiti wa zao la Kahawa(TaCRI)kanda ya Maruku mkoani Kagera,imelenga kuzalisha jumla ya miche ya kahawa zidi ya 3.5 milioni,ambayo itasambazwa kwa wakulima wa zao hilo ndani ya kanda ya ziwa Viktoria.

Akiongelea juu ya uzalishaji huo,hivi karibuni meneja wa TaCRI kanda ya ziwa bw.Nyabis Ng'homa,uzalishaji huo ni sehemu ya malengo ya taasisi hiyo kwa mwaka huu.

Bw.Ng'homa alifafanua kuwa miche hiyo imelengwa kuzalishwa katika vitalu vilivyoko katika wilaya za Bukoba vijijini,Missenyi,Muleba,Karagwe,Biharamulo na Ngara.

Vitalu vingine vitakavyosalisha miche hiyo ni katika wilaya za Ukerewe,Sengerema na Geita.Ambavyo idadi ya miche itakayokuwa imezalishwa katika vitalu hivyo inakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 3.5 ambayo itasambazwa kwa wakulima.

Wakati huo huo,wakulima mkoani hapa,wameshauriwa kujenga utamaduni wa kutembelea kituo cha utafiti wa kilimo Maruku ili kupata ushauri wa kilimo bora pamoja na mbegu bora.

Kahawa limeendelea kuwa ni zao kuu la biashara mkoani Kagera lakini hivi sasalinazidi kudorora kutokana na kupungua kwa mashina ya mibuni mashambani kutokana na mamlaka husika hususan chama cha ushirika cha KCU(1990)Ltd kutokuwa na mikakati madhubuti ya kumkaribia mkulima katika kazi yake ya kilimo cha kahawa shambani,aidha kwa mikopo nafuu na isiyo na ugumu wa kuipata.

Kwa hali hiyo wkulima washindwa kupata pembejeo kama vile samadi na nyingine mintarafu zao hilo.

Kutokana na uchumi mdogo wa wakulima hao uchunguzi umeonyesha kuwa baadhi ya mashamba ya kahawa mkoani humo yameonekana kukanda na kuonyesha kushambuliwa na wadudu kama vile sisimizi nawengine.

Tatizo kubwa ambalo linaonekana kuyakabili mashamba ya wakulima kwa sasa ni ugonjwa wa MNYAUKO wa mibuni ambapo mibuni inazidi kunyauka mashambani kila kukicha.

Pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na wataalam wa kilimo katika mkoa kwa kushirikiana na kituo cha utafiti Maruku ili kutatua tatizo hilo,kwa nafsi ya mkulima uchumi wake unahofiwa kuwa hatarini.

IJUE BUKOBA

KAHWA YANYAUKA UCHUMI WA WAKULIMA HATARINI

Vitalu vingine vitakavyosalisha miche hiyo ni katika wilaya za Ukerewe,Sengerema na Geita.Ambavyo idadi ya miche itakayokuwa imezalishwa katika vitalu hivyo
  inakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 3.5 ambayo itasambazwa  kwa wakulima.

Wakati huo huo,wakulima mkoani hapa,wameshauriwa kujenga utamaduni wa kutembelea kituo cha utafiti wa kilimo Maruku ili kupata ushauri wa kilimo bora pamoja na mbegu bora.

Kahawa limeendelea kuwa ni zao kuu la biashara mkoani Kagera lakini hivi sasalinazidi kudorora kutokana na kupungua kwa mashina ya mibuni mashambani kutokana na mamlaka husika hususan chama cha ushirika cha KCU(1990)Ltd kutokuwa na mikakati madhubuti ya
  kumkaribia  mkulima katika kazi yake ya kilimo cha kahawa shambani,aidha kwa mikopo nafuu na isiyo na ugumu wa kuipata. Kwa hali hiyo wkulima washindwa kupata pembejeo kama vile samadi na nyingine mintarafu zao hilo.Kutokana  na uchumi mdogo wa wakulima hao uchunguzi umeonyesha kuwa baadhi ya mashamba ya kahawa mkoani humo yameonekana kukanda na kuonyesha kushambuliwa na wadudu kama vile sisimizi nawengine.

Tatizo kubwa ambalo linaonekana kuyakabili mashamba ya wakulima kwa sasa ni ugonjwa wa MNYAUKO wa mibuni ambapo mibuni inazidi kunyauka mashambani kila kukicha.Pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na wataalam wa kilimo katika mkoa kwa kushirikiana na kituo cha utafiti Maruku ili kutatua tatizo hilo,kwa nafsi ya mkulima uchumi wake unahofiwa kuwa hatarini.

MWISHO

Friday, March 2, 2012

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA UTALII LEO

 Meneja wa kampuni ya utalii(KIROYELA TOURS BUKOBA) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari mkoani Kagera ambao wametembelea jengo la makumbusho eneo la Nyamkazi Manispaa ya Bukoba

RPC KAGERA ANAKEMEA UHALIFU MBELE YA VYOMBO VYA HABARI
 Jeshi la polisi mkoani Kagera limezidi kukemea vitendo vya uhalifu hasa kwa kutumia njia ya pilisi shirikishi na polisi jamii na wito huo umetolewa na kamanda wa polisi mkoani hapa Henry Salewi

HILI NI MOJA YA MABWAWA LINALOTUMIWA KWA AJILI YA UFUGAJI SAMAKI AINA YA SANGARA NA KAMBALE LILILOPO KATA MUHUTWE WILAYA YA MULEBA MKOA WA KAGERA

Thursday, March 1, 2012

MIMI NI MWANDISHI wa habari za mazingira ninaishi wilayani Bukoba mkoani Kagera, Tanzania,nimekuwa nikichunguza habari hizo nikiibua habari zihusuzo mazingira na habari nyingine za kijamii kwaajili ya maendeleo ya nchi yetu. habari na makala zangu zimesaidia sana katika kuboresha mawazo ya wananchi kiuchumi.    Mkoa wa Kagera unazo sifa kubwa kirasilmali. Kwanza hali yake ya hewa ni mvua kila msimu hazikosekani.Upo umeme wa kuaminika kutoka Jinja nchini Uganda.Mkoa unayo hazina ya watu walioelimika kkwa nyanja mbali mbali,watu hao nina imani kuwa wakiamuakuujenga mkoa hata kama wanaishi nje ya nchi hayo yanawezekana.

It is therefore beyond doubt that hence Kagera region is within the context of the central african nations,the resourceful climate and lifestyles of the people may cause drastic changes of the area. YOU are very much welcome to relay your views through this arena.